• HABARI MPYA

  Saturday, July 06, 2024

  SIMBA SC YASHUSHA KIUNGO WA SHUGHULI KUTOKA NIGERIA


  KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo mkabaji Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Rivers State kama mchezaji wake mpya wa saba kuelekea msimu ujao.
  Wengine wapya ni mabeki wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union.
  Wengine ni winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe na washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao, Abidjan na mzawa, Valentino Mashaka Kusengama (22) kutoka Geita Gold.
  Aidha, jana Simba SC jana imemtambulisha Kocha Mkuu mpya, Fadluraghman ‘Fadlu’ Davids (43) raia wa Afrika Kusini kuwa Kocha wake mpya Mkuu, akichukua nafasi ya Mualgeria Abdelhak Benchika aliyeondoka April 28, mwaka huu.
  Fadlu Davids amekuja na safu yake nzima ya Wasaisizi, wote raia wenzake wa Afrika Kusini, Kocha Msaidizi, Darian Wilken, Kocha wa Makipa, Wayne Sandilands, Kocha wa Fitness, Riedoh Berdien na Mchambuzi, Mueez Kajee.
  Kikosi kinatarajiwa kuondoka Jumatatu kwenda mjini Ismailia nchini Misri kuweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASHUSHA KIUNGO WA SHUGHULI KUTOKA NIGERIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top