// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); NI ENGLAND NA HISPANIA FAINALI EURO 2024 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE NI ENGLAND NA HISPANIA FAINALI EURO 2024 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, July 11, 2024

  NI ENGLAND NA HISPANIA FAINALI EURO 2024


  TIMU ya England imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya baada ya kutoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Uholanzi katika mchezo wa Nusu Fainali usiku wa jana Uwanja wa BVB Jijini Dortmund nchini Ujerumani.
  Uholanzi walitangulia kupata kupitia kwa kiungo mshambuliaji kwenye asılı ya Surinam, Xavi Quentin Shay Simons wa Paris Saint-Germain dakika ya saba, kabla ya Nahodha na mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Edward Kane kuisawazishia England kwa penalti dakika ya 18 kufuatia kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham kuchezewa rafu na beki wa Inter Milan, Denzel Dumfries.
  Shujaa wa England alikuwa ni mshambuliaji wa Aston Villa, Oliver George Arthur Watkins aliyeifungia Three Lions bao la ushindi dakika ya 90 na sasa itakutana na Hispania katika Fainali Jumapili Uwanja wa Olympia Jijini Berlin.
  Mara ya kwanza na ya mwisho England kufika Fainali ya Euro ilikuwa mwaka 2020 wakiwa wenyeji na wakafungwa kwa penalti 3-2 na Italia kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Wembley Jijini London.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NI ENGLAND NA HISPANIA FAINALI EURO 2024 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top