• HABARI MPYA

  Thursday, July 04, 2024

  TAIFA STARS YAPANGWA NA DRF, GUINEA NA ETHIOPIA KUWANIA TIKETI YA AFCON 2025

  TANZANIA imepangwa Kundi H pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Guinea na Ethiopia kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Morocco mwaka 2025.
  Katika Droo iliyopangwa leo Jijini Johannesburg, Afrika Kusini, mabingwa watetezi, Ivory Coast wamepangwa Kundi G pamoja na Zambia, Sierra Leone na Chad.
  Jumla ya 52 zinatarajiwa kushiriki hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya AFCON 2025 kuanzia Septemba 2 hadi Novemba 19 mwaka huu na washindi wawili wa makundi yote 12 watatengeneza idadi ya timu 24 wakiwemo wenyeji Morocco, kufuzu AFCON ya mwakani.

  MAKUNDI YOTE KUFUZU AFCON 2025 MOROCCO
  Kundi A: Tunisia, Madagascar, Comoros, Gambia
  Kundi B: Morocco, Gabon,Central Africa Republic, Lesotho 
  Kundi C: Egypt, Cape Verde, Mauritania, Botswana
  Kundi D: Nigeria, Benin Libya, Rwanda 
  Kundi E: Algeria, Equatorial Guinea, Togo, Liberia
  Kundi F: Ghana, Angola, Sudan, Niger
  Kundi G: Cote d'Ivoire, Zambia, Sierra Leone, Chad
  Kundi H: DR Congo, Guinea, Tanzania, Ethiopia
  Kundi I: Mali, Mozambique, Guinea Bissau, Eswatini
  Kundi J: Cameroon, Namibia, Kenya, Zimbabwe
  Kundi K: South Africa, Uganda, Congo, South Sudan
  Kundi L: Senegal, Burkina Faso, Malawi, Burundi


  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAIFA STARS YAPANGWA NA DRF, GUINEA NA ETHIOPIA KUWANIA TIKETI YA AFCON 2025 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top