• HABARI MPYA

  Wednesday, July 10, 2024

  JOHN BOCCO NA CHARLES ILANFYA WAJIUNGA NA JKT TANZANIA


  KLABU ya JKT Tanzania ikmmetambulisha mshambuliaji mkongwe, John Raphael Bocco (34) aliyeachwa na Simba kuwa mchezaji wake mpya pamoja na winga, Charles Martin Ilanfya (21) kutoka Mtibwa Sugar iliyoshuka daraja.
  Bocco aliibukia Cosmopolitan ya mwaka 2005, kabla ya kuhamia Azam FC mwaka 2007 ikiwa Daraja la Kwanza na mabao yake ndiyo yaliipandsha Ligi Kuu msimu wa 2008-2009 na akacheza timu hiyo hadi mwaka 2017 alipohamia Simba SC aliyoichezea hadi msimu uliopita.
  Kwa upande Ilamfya aliibukia Mwadui FC ya Shinyanga mwaka 2018 hadi 2019 akaenda KMC, 2020 akahamia Simba SC, ambayo baada ya nusu msimu ilimrudisha KMC kwa mkopo, 2022 akaenda Mtibwa Sugar alikocheza hadi Mei mwaka timu hiyoiliposhuka Daraja.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JOHN BOCCO NA CHARLES ILANFYA WAJIUNGA NA JKT TANZANIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top