• HABARI MPYA

  Wednesday, July 10, 2024

  AZAM FC YATHIBITISHA KUMUUZA KIPRE JUNIOR MC ALGER


  KLABU ya Azam FC imethibitisha kumuuza winga Muivory Coast, Kipré Tiagori Emmanuel Junior Zunon (24) kwa klabu ya Mouloudia Club d'Alger, inayofahamika zaidi kama MC Alger au MCA kwa kifupi ya Algeria.
  Taarifa ya Azam FC imesema; “Tumefikia makubaliano na klabu ya MC Alger ya Algeria kumuuza kiungo mshambuliaji wetu, Kipre Junior,”.
  Taarifa hiyo imeongeza; “Kipre Jr, tayari ameshasaini mkataba wa miaka minne na klabu hiyo baada ya kufaulu vipimo vya afya.”
  Aidha, Azam FC imemshukuru Kipre Junior kwa mchango wake ndani ya klabu hiyo kwa misimu yake miwili na imemtakia kila la kheri katika klabu yake mpya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YATHIBITISHA KUMUUZA KIPRE JUNIOR MC ALGER Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top