• HABARI MPYA

  Tuesday, July 02, 2024

  SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI MGANDA WA ASANTE KOTOKO


  KLABU ya Simba imemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana, ambaye aliibukia Vipers SC kabla ya kupelekwa kwa mkopo Maroons FC, zote za kwao, Uganda.
  Steven Mukwala anakuwa mchezaji mpya wa tatu Simba SC baada ya beki mzawa, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga na winga Mzambia, Joshua Mutale kutoka Power Dynamos ya kwao.
  Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuingia kambini wiki hii nchini Misri kujiandaa na msimu mpya, ambao utafunguliwa kwa Tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI MSHAMBULIAJI MGANDA WA ASANTE KOTOKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top