// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA SC YASAJILI ALIYEKUWA ANACHEZA LİGİ YA AFRİKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA SC YASAJILI ALIYEKUWA ANACHEZA LİGİ YA AFRİKA KUSINI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
 • HABARI MPYA

  Thursday, July 04, 2024

  SIMBA SC YASAJILI ALIYEKUWA ANACHEZA LİGİ YA AFRİKA KUSINI


  KLABU ya Simba imemtambulisha beki wa kati mzawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini kuwa mchezaji wake mpya wa tano kuelekea msimu ujao.
  Hamza ni mchezaji aliyeibukia Mbeya City mwaka 2020, kabla ya kuhamia KMC mwaka 2021 na Namungo FC 2022 ambayo ilimuuza SuperSport mwaka jana.
  Wachezaji wengine waliosajiliwa Simba ni beki mzawa, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union, winga Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya Zambia na washambuliaji Mganda, Steven Mukwala (24) kutoka Asante Kotoko ya Ghana na Muivory Coast, Jean Charles Ahoua (22) kutoka Stella Club d'Adjamé ya kwao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YASAJILI ALIYEKUWA ANACHEZA LİGİ YA AFRİKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top