• HABARI MPYA

  Wednesday, July 10, 2024

  HISPANIA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA UFARANSA 2-1


  TIMU ya Hispania imefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ufaransa katika mchezo wa Nusu Fainali mbele ya mashabiki 62,042 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich nchini Ujerumani.
  Ufaransa waliuanza mchezo vizuri na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na mshambuliaji wa  Paris Saint-Germain, Randal Kolo Muani (25) mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya nane.
  Lakini kinda wa Barcelona mwenye umri wa miaka 16, Lamine Yamal Nasraoui Ebana ambaye baba yake ni Mmorocco na mama yake anatokea Equatorial Guinea akaisawazishia Hispania kwa shuti la mbali dakika ya 21.
  Aliyeihakikishia Hispania tiketi ya Fainali ni mshambuliaji wa RB Leipzig, Daniel Olmo Carvajal mwenye umri wa miaka 26 baada ya kufunga bao la ushindi dakika ya 25.
  Nusu Fainali ya mwisho ya Euro 2024 inachezwa Leo Saa 4:00 usiku Uwanja wa Westfalenstadion Jijini Dortmund.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: HISPANIA YATOKA NYUMA NA KUICHAPA UFARANSA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top