• HABARI MPYA

  Wednesday, August 16, 2017

  RONALDO ASHINDWA RUFAA, ZIDANE 'MAPOVU' YAMTOKA, ADAI NI UONEVU

  Cristiano Ronaldo alionyeshwa kadi ya njano kwa kuvua jezi akamsukuma refa kwa hasira baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


  MECHI TANO AMBAZO RONALDO ATAZIKOSA 

  Agosti 16 - vs Barcelona (home) -marudiano Super Cup ya Hispania
  Agosti 20 - vs Deportivo (away)
  Agosti 27 - vs Valencia (home)
  Septemba 9 - vs Levante (home)
  Septemba 17 - vs Real Sociedad (away)
  SHIRIKISHO la Soka Hispania limeshikilia msimamo wa kumsimaamisha kwa mechi tano, Cristiano Ronaldo.
  Ronaldo alifungiwa mechi moja baada ya kutolewa nje kwenye mchezo wa kwanza wa Super Cup ya Hispania na akaongezewa kifungo cha mechi nne kwa kumsukuma refa Ricardo de Burgos nyuma baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu.
  Nyota huyo wa Real Madrid ataukosa mchezo wa marudiano wa Super Cup ya Hispania dhidi ya mahasimu, Barcelona usiku wa Jumatano na mechi nyingine nne za mwanzo za La Liga, kuanzia wa Real Madrid dhidi ya Deportivo La Coruna Jumapili.
  Madrid ikaikatia rufaa kadi ya pili ya njano ya Ronaldo katika mechi hiyo ambayo walishinda 3-1 dhidi ya Barcelona, ambayo mshambuliaji huyo wa Ureno alionyeshwa kwa kujiangusha. 
  Kocha wa Madrid, Zinedine Zidane amehoji uamuzi wa Shirikisho la Soka Hispania kumfungia Ronaldo mechi tano.  
  "Tunachofanya ni kusubiri kesho," Zidane amesema. "Kamati itaakutana asubuhi. Baadsa ya hapo, tutaona nini cha kufanya. Nimesikitishwa. wote kati yetu tumesikitishwa sana. Kama kawaida yangu, siwezi kuwazungumzia marefa,". 
  "Tutazungumza vizuri na Kamati juu ya hili. Unapofikiria (Ronaldo) hatacheza mechi tano kwetu, kitu fulani kikubwa.
  Inanisumbua na inatusumbua wote. Ni mechi nyingi kwake, ni hayo gtu ninayoweza kusema,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RONALDO ASHINDWA RUFAA, ZIDANE 'MAPOVU' YAMTOKA, ADAI NI UONEVU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top