• HABARI MPYA

  Thursday, August 17, 2017

  JENGO LA YANGA MAKAO MAKUU JANGWANI KUPIGWA MNADA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WIZARA ya Ardhi Maendeleo ya Makazi imetangaza kulipiga mnada jengo la klabu ya Yanga, makao makuu makutano ya mitano ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam kesho. 
  Katika tangazo lililotoka kwenye gazeti la leo, Wizara ya Ardhi imesema hatua hiyo inafuatia kesi iliyofunguliwa na Kamishna wa Ardhi katika Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya na Temeke na Ilala dhidi ya Yanga.
  Na kwa mujibu wa tangazo la kampuni ya udalali ya Msolopa Investmenst Limited, mnada huo utaanza Saa 4:00 asubuhi ya kesho hapo hapo Jangwani.
  Makao makuu ya Yanga yatapigwa mnada kesho kuazia Saa 4:00 asubuhi

  Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba ameshitushwa na tangazo hilo kwa kuwa tayari wapo katika jitihada za kulipa madeni yao.
  “Ni kweli tuna deni kubwa tunadaiwa la ardhi, lakini tayari tulifanya nao mazungumzo na kukubaliana namna ya kulilipa kupitia mapato yetu ya milangoni. Lakini tu tatizo ni kwamba hapa katikati Ligi ilisimama, lakini hivi karibuni inaanza na tutaendelea kulipa,”amesema.
  Lakini kwa kuwa hatua ya kulipiga mnada jengo hilo imekwishatangazwa, Mkwasa amesema kwamba atawasiliana na Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga ili azuie zoezi hilo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: JENGO LA YANGA MAKAO MAKUU JANGWANI KUPIGWA MNADA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top