• HABARI MPYA

  Wednesday, August 16, 2017

  PASHA PASHA YA LIGI KUU...MWADUI YAIFUMUA PAMBA 5-3 NYAMAGANA

  Na Mwandishi Wetu, MWANZA
  KATIKA kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Mwadui FC leo imeteremka Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza na kumenyana na wenyeji, Pamba FC katika mchezo wa kirafiki.
  Katika mchezo huo, Mwadui FC imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Pamba inayojiandaa na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara nayo.
  Mabao ya Mwadui FC yamefungwa na Salim Khamis, Awadh Juma kila mmoja mawili na lingine Nyanda Babi, wakati ya Pamba yamefungwa na Peter Magata, Meshack Kikona kwa penalti na Peter Aguero.
  Baada ya mchezo huo, kocha Mkuu wa Mwadui FC, Jumanne Ndambi amekisifu kikosi cha Pamba na kusema kitafanya vema katika Ligi Daraja la Kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PASHA PASHA YA LIGI KUU...MWADUI YAIFUMUA PAMBA 5-3 NYAMAGANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top