• HABARI MPYA

  Tuesday, August 01, 2017

  KAREKEZI KOCHA MPYA WA RAYON SPORTS, ATASAIDIWA NA KATAUTI

  MSHAMBULIAJI wa zamani wa Rwanda, Olivier Karekezi ameteuliwa kuwa kocha mabingwa wa sasa, Rayon Sports kwa mkataba wa miaka miwili. 
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 tu, aliyetamba katika klabu ya APR, ataanzia rasmi kazi ya ukocha kwa wapinzani, Rayon, akichukua nafasi ya Djuma Masudi, aliyejiuzulu muda mfupi tu baada ya kuipa timu hiyo taji la ligi msimu uliopita. 
  Baada ya kucheza timu kadhaa Sweden, Karekezi alistaafu soka na kupaya mafunzo ya ukocha kabla ya kuchukuliwa na Rayon yenye maskani yake mjini Kigali. 
  Olivier Karekezi ndiye kocha mpya mabingwa wa Rwanda, Rayon Sports 

  "Nina furaha kuwa nyumbani na kuanza kazi kama kocha wa Rayon Sports, lakini muhimu zaidi, tunataka kucheza soka nzuri na kushinda mataji. Pamoja na kwamba Ulaya nilikuwa nikifundisha timu za vijana chini ya umri wa miaka 17, lakini nafikiri naweza kusogea kwenye timu ya wakubwa na kufanya vizuri,". 
  "Wakati nilipokuwa mchezaji, sikuwa nafikiria chochote zaidi ya ushindi na hiyo imeendelea kuwa na falsafa yangu hata nilipoanza kufundisha. Falsafa yetu inapaswa kuwa kucheza soka nzuri na kushinda mataji naRayon Sports,". 
  "Nimecheza APR na sasa ni kocha wa Rayon Sports. Mimi ni kocha kitaaluma na ninachotaka ni kufanya kazi yangu kwa usahihi,”amesema Karekezi, aliyewasili Kigali Alhamisi iliyopita kusaini mkataba. 
  Mshambuliaji huyo mwenye bahati amecheza soka ya kulipwa katika nchi za Sweden, Norway na Tunisia na alikuwemo kwenye kikois cha Rwanda kilichofuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2004 nchini Tunisia na ameng'ara Amavubi kati ya mwaka 2000 na 2013. 
  Katika klabu ya Rayon, atasaidiwa na wachezaji wenzake wa zamani wa Amavubi, Kocha Msaidizi Hamadi ‘Katauti’ Ndikumana na Kocha wa makipa, Ramadhan Nkunzingona, wakati Marcel Lomami atakuwa kocha wa mazoezi ya kuujenga mwili.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAREKEZI KOCHA MPYA WA RAYON SPORTS, ATASAIDIWA NA KATAUTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top