• HABARI MPYA

    Saturday, May 19, 2012

    NI SIKU KUBWA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA LEO


    Drogba is desperate to finally win Champions League
    WA KUMULIKWA LEO... Drogba anatarajia kuaga kwa ushindi na taji Stamfrod Bridge.
    Published: Today at 00:06

    NI siku kubwa katika ulimwengu wa soka — huku watazamani wapatao Milioni 300 wakishuhudia mechi kupitia Televisheni na kiasi cha pauni Milioni 140 ndani ya mechi mbili...

    Mchana huu kuna kiasi cha pauni Milioni 90 kutokana na mechi kati ya Blackpool na West Ham, fainali ya Daraja la Kwanza, Championship.
    Kisha, usiku, Chelsea wanapigania pauni Milioni 50 kuifunga Bayern Munich katika fainali ya Ligi ya Mabingwa.
    Mechi hizo zote kwa ujumla zitavutia watazamani wa TV zaidi ya Milioni 300—  huku wengi zaidi wakitega macho yao katika mechi ya Ujerumani.
    Mabingwa wa mwaka jana, Barcelona waliingiza zaidi ya pauni Milioni 43 kutokana na zawadi na mapato ya TV.
    Chelsea watakusanya pauni Milioni 7.6 kwa zawadi pekee, iwapo watatwaa ubingwa au pauni Milioni 5.5 wakifungwa.
    Kiasi cha fedha za zawadi ambazo wamekwishatia kibindoni hadi sasa ni zaidi ya pauni Milioni 11 — pauni Milioni 3.6 kwa kutinga Nusu Fainali, pauni Milioni 2.8 Robo Fainali, pauni Milioni 2.5 kwa hatua ya 16 Bora, pauni Milioni 2.02 kwa mechi tatu za makundi walizoshinda na pauni 675,000 kwa sare zao mbili hatua ya makundi.
    Bosses Holloway and Allardyce with Championship play-off trophy
    TAJI LA PAUNI MILIONI 90... Makocha Holloway na Allardyce wanaochuana katika fainali ya  Championship
    Mechi ya Championship kati ya Blackpool na West Ham kwenye Uwanja wa Wembley inatarajiwa kuvutia watazamaji Milioni 5.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: NI SIKU KUBWA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top