Last Updated: 19th May 2012
VIMWANA wa kujirusha walimteka Wayne Rooney ambaye anajiandaa na Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2012 na kujiachia naye katika klabu moja la usiku mjini Las Vegas.
Alicheza nao na kupiga nao stori sana mashabiki hao wa kike wenye mvuto wa kingono hadi saa 9, wakati huo mkewe, Coleen amelala katika hoteli yao.
Mshambuliaji wa England, Wayne alianza kuwindwa na vimwana mara tu alipoingia kwenye klabu hiyo.
Kundi fulani la wasichana hatimaye lilifanikiwa kumteka na kuketi naye, wakinywa na kupiga stori hadi 'mida mobovu'.
Mtu mmoja aliyekuwa klabu alisema: “Wayne na kundi lake waliingia kama saa 7 usiku katika casino la hoteli hiyo.
“Alikuwa anafurahia kuzungukwa na wanawake. Alikuwa amezungukwa na vimwana babu kubwa. Lilikuwa bonge la sherehe kwao na mavinywaji kibao.
Nyota wa Manchester United, Wayne mwenye umri wa miaka 26, yupo Las Vegas na mkewe Coleen na mtoto wao wa kiume Kai, kujiachia kabla ya kwenda Euro 2012 na baada ya kumaliza msimu mgumu wa Ligi Kuu England.
Coleen mwenye umri wa miaka 26, hakutoka na Wayne Ijumaa ya jana kwenda klabu ya Tryst, ambayo ipo katika hoteli waliyofikia.
Katika kundi hilo, Wayne alikuwa pia na mchezaji mwenzake wa zamani wa Man Utd, Wes Brown na mkewe Leanne.
Mapema Wayne na Coleen walijiachia kwenye pool la hoteli hiyo na mama yake, Colette na marafiki.


.png)
0 comments:
Post a Comment