Saturday's gossip column
SPURS KUACHANA NA MGONJWA WA MOYO
KLABU ya Tottenham inaweza kuachana na mpango wa kumchukua kwa pauni Milioni 18, mshambuliaji wa Marseille, Loic Remy kwa sababu ya hofu kwamba mwanasoka huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25 anaweza kuwa na matatizo ya moyo.
VAN PERSIE REAL, BARCA AU CITY...
MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Robin van Persie kutaka kwake mshahara mkubwa kunaweza kumfanya ahamie Real Madrid, Barcelona na Manchester City.
KLABU ya Manchester City inaelezwa kwamba ipo kwenye uchunguzi wa uhalali wa kuuziwa kwa pauni Milioni 28, mshambuliaji wa Athletic Bilbao, Fernando Llorente, ambaye amefunga mabao 29 katika mechi 51 msimu huu.
MCHEZAJI anayetakiwa na Manchester United, Kevin Strootman, kinda wa miaka 22 wa klabu ya PSV anayecheza nafasi ya kiungo, anajiandaa kuanza mazungumzo na AC Milan.
KLABU ya Lille inajiandaa kuanza mazungumzo ya mkataba na mchezaji mwenye thamani ya pauni Milioni 35, Eden Hazard, ambaye anatakiwa na Manchester United na Manchester City.
QPR inamtaka kipa wa West Ham, Robert Green ikiwa The Hammers watafeli kurejea Ligi Kuu leo wakichezsa mechi ya mwisho ya mchujo ya Championship.
WINGA wa Manchester City, Adam Johnson inafikiriwa anatafakari mustakabali wake na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu England, baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha England kinachokwenda Euro 2012.
LIVERPOOL YAMRUDIA BENITEZ
KLABU ya Liverpool imemtongoza kocha wake wa zamani, Rafael Benitez baada ya Brendan Rodgers kukataa ofa ya kuzungumza na klabu hiyo ya Anfield ili kujaza nafasi ya ukocha katika klabu hiyo, ambayo iko wazi.
WAKATI HUO HUO: Wekundu wa Anfield wanajiandaa kumpa Luis Suarez ofa ya ongezeko la asilimia 25 katika mshahara wake ili kumzuia asiondoke.



.png)
0 comments:
Post a Comment