• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 27, 2009

  SIMBA YANOA MAKUCHA KWA JKT RUVU KESHO

  TIMU ya Simba kesho inapambana na JKT Ruvu katika mchezo wa kirafiki wa kusherekea ufunguzi wa uwanja wa Kinesi.
  Katibu Mkuu wa Chama Cha soka Wilaya ya Kinondoni KIFA, Frank Mchaki alisema jana kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekamilika, unatarajiwa kuanza saa 10 jioni.
  Pambano hilo litakuwa la tatu kwa timu hizo kumenyana, katika pambano la mzunguko wa kwanza wa ligi Kuu ya Tanzania bara, JKT Ruvu walishinda bao 1-0 wakati katika mchezo wa marudiano Simba ilishinda mabao 2-1.
  Hivyo pambano la leo linatarajiwa kuwa gumu, timu ya Simba itawakosa wachezaji wake sita walioko na kikosi cha timu ya Taifa kinachoshiriki fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN), JKT itamkosa kiungo Moshi Kazimoto aliyeitwa kwa mara ya kwanza kwenye kikosi hicho.
  Akizungumzia mchezo huo, kocha mkuu wa klabu ya Simba, Mzambia Patrick Phiri alisema kuwa mchezo wa leo licha ya sherehe ya uzinduzi wa uwanja wa Kinesi pia atatumia kuangalia kikosi chake kwa ajili ya michezo saba ya ligi kuu iliyosalia
  “Mchezo huu pia nitautumia kama maandalizi ya ligi Kuu iliyokuwa imesimama, nitafahamu nibadilishe nini, nifanya nini, wachezaji wangu wamejiandaa kwa kiasi gani” alisema Phiri.
  Ligi Kuu ya soka Tanzania bara inatarajiwa kuanza Machi 14 katika viwanja mbalimbali, hadi sasa timu ya Yanga ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA YANOA MAKUCHA KWA JKT RUVU KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top