• HABARI MPYA

  Tuesday, February 24, 2009

  CHAN NI MASHINDANO MAGUMU- NSAJIGWA

  na abdul mohammed, abidjan
  NAHODHA wa timu ya taifa, Shadrack Nsajigwa amesema kwamba michuano ya CHANinayoendelea nchini Ivory Coast ni migumu na iko katika kiwango cha juu.Akizungumza juzi mara tu baada ya mechi kati ya Stars na Senegal ambayo ilimalizika kwa Stars kulala kwa bao 1-0, Nsajigwa alisema kwamba michuano hiyo ni tofauti na ile ya klabu bingwa, Afrika Mashariki na Kati (CECAFA)waliyoizoea."Hapa kuna ugumu kuanzia kwenye kufuzu hadi kufikia hatua hii ya fainali, unakutana na timu ngumu ambazo zimefanya kazi kubwa hadi kufuzu," alisema Nsajigwa.Aliongeza kwamba hata taratibu za kufuzu michuano ya CHAN ni ngumu ukilinganisha na ile ya CECAFA na kwamba hata michuano iko katika kiwango cha juu.Hata hivyo Nsajigwa alisema kwamba anaamini bado wana nafasi ya kupamabana hadihatua ya mwisho katika mechi mbili zilizobaki kabla ya kujua hatima yao ya kusonga mbele au kuziaga fainali.Stars itajitupa uwanjani kesho kuumana na wenyeji Ivory Coast ambao wana hasira za kufungwa mabao 3-0 na Zambia kabla ya kutupa karata yake ya mwisho katika mechi ya Kundi B dhidi ya Zambia hapo Jumamosi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHAN NI MASHINDANO MAGUMU- NSAJIGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top