• HABARI MPYA

    Friday, February 27, 2009

    STARS NI KUFA NA KUPONA KWA ZAMBIA


    Kikosi cha Stars juu kabisa na Zambia chini, kesho kazi ipo

    TIMU ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kesho inatupa karata yake ya mwisho ya kundi Akatika mechi muhimu dhidi ya Zambia.Stars itahitaji kushinda mechi ya leo ili iweze kusonga mbele na mojawapo vinginevyomatokeo ya sare yanaweza kuikwaza timu hiyo iwapo Senegal itaifunga au kutoka sarena Ivory Coast katika mechi nyingine ya leo.Kocha wa Stars, Marcio Maximo anatambua ugumu wa mechi ya leo na tayari amewaandaawachezaji wake katika hilo.Akizungumza jana, Maximo alisema kwamba anajivunia timu yake ambayo alisemawachezaji wake wengi wameonyesha kujituma na kufuata maelekezo yake.Maximo alijivunia safu yake ya ulinzi wa kati akisema kwamba Salum Sued na NadirHaroub Cannavaro wanaushirikiano mzuri ambao ulekuwa kiwazo kwa timu pinzani.Safu hiyo ya ulinzi ya Stars itakuwa na kazi ngumu ya kumdhibiti Given Sungulumaambaye tayari ana mabao matatu aliyoyafunga katika mechi ya kwanza dhidi ya wenyejiIvory Coast.Singuluma katika mechi hiyo ndiye qliyekuwa nyota wa mchezo na bila shaka kinaCannavaro na Sued watakuwa na kazi ngumu ya kumdhibiti mchezaji huyo.Mbali na Sinfguluma nyota mwingine wa Zambia atakayeiweka Stars katika wakati mgumuni pamoja na Sakuwa Jonas na Kebby Hachipuka.Kwa upande wake Stars bila shaka itatumia kikosi kile kile kilichoifunga Ivory Coastbao 1-0 jumatano iliyopita.Mechi ya leo ya Stars inachezwa katika mji wa Bouake, mji ambao pia ni maarufu kwasoka na ndiko anakotokea beki wa Arsenal, Kolo Toure na nduguye Yaya.Stars kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika kundi hilo ikiwa na pointi tatu na baomoja, vinara wa kundi hilo ni Zambia wenye pointi nne na mabao matatu wakifuatiwa naSenegal wenye pointi nne na bao moja wakati Ivory Coast inashika mkia na tayariimeziaga fainali hizo baada ya kufungwa na Tanzania.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: STARS NI KUFA NA KUPONA KWA ZAMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top