• HABARI MPYA

  Jumanne, Februari 03, 2009

  AMBANI WA YANGA AGEUKIA FILAMU


  MSHAMBULIAJI hatari wa mabingwa wa soka nchini, Yanga ya Dar es Salaam, Boniphace Ambani, amejiingiza katika uigizaji wa filamu na sasa ataonekana katika movie mpya ijulikanayo kama Domestic Love.
  Mmoja ya wasanii walioshiriki katika filamu hiyo, Flora Mvungi, alisema kwamba Ambani amecheza kama mhusika mkuu, akiwa ni kijana mwenye uwezo wa kifedha aliyemuona msichana anayetokea familia masikini.
  “Filamu hii inafanywa na kampuni moja kutoka Kenya inaitwa Victoria Production, hawa jamaa ni wapya na ndiyo kwanza wanaanza mambo haya, lakini wana vifaa vya kisasa na wanaonekana wamepania kufanya kazi kwa ubora.
  “Kwa sasa tupo kambini Lunch Time Hotel na tumeshaanza kupiga picha. Tunatarajia hadi mwezi ujao, filamu iwe tayari sokoni,” alisema binti huyo, ambaye pia amecheza filamu kadhaa.
  Akizungumzia maudhui ya filamu hiyo, Flora ambaye amecheza kama mke wa Ambani, alisema ni simulizi ya kimapenzi, inayopelekea mumewe huyo kujikuta akilazimika kutembea na ndugu yake yeye, kutokana na matatizo ya mke wake (yaani Flora).
  Msichana huyo ameshacheza filamu na michezo kadhaa kabla ya kuigiza filamu hiyo akiwa na Ambani. Ndiye anayeonekana katika mchezo maarufu wa Bongo Dar es Salaam, unaoonyeshwa na kituo cha TBC1 akishirikiana utapeli na msanii mwingine aitwaye Dude.
  Pia ameshiriki kucheza filamu za Simu ya mkononi, Harusi ya Ankara na Safari ya Amerika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AMBANI WA YANGA AGEUKIA FILAMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top