• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 02, 2009

  SIMBA SARE, YANGA UBINGWA HUOOOOOO


  Mgosi kushoto akishangilia na Jabir Aziz


  SIMBA ya leo imebanwa katika Uwanja wa nyumbani, Taifa mjini Dar es Salaam kwa sare ya 1-1 na JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  JKT inayonolewa na Charles Kilinda ilitangulia kupata bao dakika ya 41, mfungaji akiwa ni Haroun Adolph kabla ya Mussa Hassan Mgosi, kumuokoa kocha wake, Mzambia Patrick Phiri katika dakika ya 65.
  Mgosi alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti, baada ya mchezaji mmoja wa JKT kudaiwa kuunawa mpira kwenye eneo la hatari. Sare hiyo imezidi kuwatengenezea mazingira mazuri watani wao wa jadi, kutwaa ubingwa mapema zaidi msimu huu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SARE, YANGA UBINGWA HUOOOOOO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top