• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 11, 2009

  Gofu ya Zain Lugalo Fiddle kurindima leo

  WACHEZAJI gofu wapatao 60 kutoka klabu mbalimbali wanatarajiwa kuchuana katika mashindano ya kila wiki ya Zain/Lugalo Fiddle kwenye Uwanja wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo leo (Februari 11, 2009).
  Mashindano hayo ya kila wiki, yanatarajiwa kuanza mchana, na baadaye jioni kutatolewa zawadi anuwai kwa washindi ikiwa ni pamoja na simu selula zinazotolewa na wadhamini wa mashindano hayo, kampuni ya simu za mkononi ya Zain Tanzania.
  Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania , Beatrice Singano alisema Dar es Salaam jana kuwa Zain imesaini mkataba wa miaka mitatu kudhamini mashindano ya Kombe la Mkuu wa Majeshi katika klabu ya gofu ya Lugalo, ili kusaidia kuinua kiwango cha michezo nchini.
  "Zain inaona fahari kudhamini mashindano ya kila wiki ya gofu ambayo yanawakutanisha pamoja wachezaji gofu wa ridhaa kwa ajili ya michezo na burudani, na tunatumaini idhamini wetu utaisaidia kuinua kiwango cha mchezo huo.
  "Tunatumaini udhamini wetu si kwamba utaongeza tu chachu ya ushindani na kujenga afya za wachezaji, lakini pia utasaidia kuendeleza na kuinua michezo ya Tanzania kwa ujumla.
  Nahodha wa klabu ya gofu ya Lugalo, Koplo Priscus Nyoni aliishukuru Zain kwa kudhamini mashindano hayo ya gofu ya kila wiki, na akabainisha lengo la mashindano hayo ni kukuza na kuendeleza mchezo wa gofu kwa kila rika, na kila wiki uwanja unakuwa wazi kwa kila mtu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: Gofu ya Zain Lugalo Fiddle kurindima leo Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top