• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 25, 2009

  AL AHLY YAPATA PIGO, YANGA CHEREKO  CAIRO, Misri
  WASWAHILI wanasema adui muombee njaa, naam bila shaka hizi zitakuwa habari njema kwa mashabiki na wapenzi wa Klabu ya Yanga ya Dar es Salaam.
  Wapinzani wa Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika, Al Ahly ya Misri Jumapili walipata pigo baada ya kiungo wake tegemeo, Mohamed Aboutrika (PICHANI JUU) kuumia kifundo cha mguu wake katika mechi dhidi ya Petrojet, iliyomalizika kwa sare ya 2-2 ugenini.
  Kwa sababu hiyo, Mohamed Aboutrika ataanza kuwa benchi akiuguza maumivu yake ambayo yamekuwa yakijirudia tangu kuanza kwa mwaka huu.
  Pamoja na sare hiyo, Ahly bado inashikilia usukani wa Ligi ya nchi hiyo, ikiwa na pointi 40, wakati Petrojet wana 35 wakiwa n nafasi ya pili.
  Wenyeji walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Ahmed Shaaban dakika ya 59 wakati kipa wa Ahly, Amir Abdul-Hamid aliposhindwa kuzuia mpira dhaifu wa adhabu uliopigwa na mchezaji huyo.
  Beki wa kushoto wa Petrojet, Osama Mohamed, alijifunga dakika ya 63 kabla ya winga wa kimataifa wa Angola, Gilberto kufunga bao la pilli kwa mabingwa wa Afrika.
  Hata hivyo, kosa lingine lilofanywa na Abdul-Hamid liliwazawadia bao la kusawazisha Petrojet lililofungwa na Amr Hassan dakika za lala salama.
  Katika mechi nyingine zilizochezwa Jumapili, Asyut Petroleum ilishinda 2 -1 dhidi ya Talaea El Geish, Ismailia iliilaza 1 - 0 Al Olympi Ghazl Al Mehalla ilitoka sare ya 1 - 1 na ENPPI, El Ittihad Al Sakandary ililazimishwa sare ya bila kufungana na Tersana SC, Itthad Al Shourta ilifungw anyumbani 2-0 na Haras El Hedood.
  Ligi hiyo iliendelea Jumatatu juzi wakati Al Moqawloon Al Arab ilipolazimishwa sare ya 1 – 1 na El Masry Club, kama ilivyokuwa kwa
  Zamalek SC dhidi ya Al Masria Lell Etesalat pia ilibanwa kwa sare ya aina hiyo.
  Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea kesho, wakati Al Ahly itakuwa mwenyeji wa Ismailia, Haras El Hedood itaikaribisha Ghazl Al Mehalla, ENPPI itakuwa mwenyeji wa El Ittihad Al Sakandary, Talaea El Geish itakuwa mwenyeji wa Itthad Al Shourta, Al Olympi itaikaribisha Asyut Petroleum.
  Ismailia pia ipo kwenye kinyang’anyiro cha ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri pia ikiwa inashika nafasi ya tatu, kwa pointi zake 35.
  Yanga na Ahly zitaanzia mjini Cairo, kati ya Machi 13 na 15, mwaka huu kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Dar es Salaam katika Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AL AHLY YAPATA PIGO, YANGA CHEREKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top