• HABARI MPYA

  Alhamisi, Februari 26, 2009

  DIHILE, NIZAR WACHUKULIWA VIPIMO CHAN

  Dihile (kushoto) hapa akiogolea na Erasto Nyoni, wote wa Ivory Coast na Stars


  WACHEZAJI wawili wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, inayoshiriki Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) mjini hapa, kipa Shaaban Dihile na kiungo Nizar Khalfan, juzi walichukuliwa na maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili kupimwa kama wanatumia dawa haramu michezoni.Kwa mujibu wa Msemaji wa CAF, Kabula Mwana Kabula, wachezaji hao walipimwa iwapo wanatumia dawa za kuongeza nguvu au dawa za kulevya na hadi leo jioni hakuna majibu yaliyowekwa hadaharani.Dihile na Nizar, waliong'ara kwenye mechi dhidi ya wenyeji Ivory Coast ambayo Tanzania ilishinda 1-0 juzi, wanaungana na wenzao, Mrisho Ngassa na Mwinyi Kazimoto waliopimwa baada ya mchezo wa kwanza dhidi ya Senegal. Tanzania ilifungwa 1-0 na Senegal.Tanzania inatarajiwa kutpa kete yake ya mwisho, Jumamosi kwa kucheza na Zambia inayoongoza kundi hilo, ikiwa na pointi nne sawa na Senegal, lakini yenyewe ina mabao mengi (matatu) ya kufunga wakati Senegal ina moja tu.Senegal itamaliza na Ivory Coast, ambayo imefungwa mechi zote mbili, kwanza na Zambia 3-0 baadaye 1-0 na Tanzania, mechi ambayo itaanza na kumalizika pamoja na ile ya Stars na Zambia. Ili ikate tiketi ya kuingia fainali, Tanzania italazimika kuifunga Zambia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: DIHILE, NIZAR WACHUKULIWA VIPIMO CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top