• HABARI MPYA

  Jumatano, Februari 18, 2009

  MAXIMO ATAJA KIKOSI CHA CHAN

  Kocha Mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo amewaacha Uhuru Suleiman, Jabir Aziz, Salvatory Ntebe na Zahor Pazi katika kikosi cha timu yake kitakachoondoka keshon kwenda nchini Ivory Coast kushiriki fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), zinazotarajia kuanza Februari 22, mwaka huu.
  Awali Maximo alitangaza kikosi cha wachezaji 27, walioingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Zimbabwe uliomalizika kwa sare ya bila kufungana.
  Shirikisho la soka barani Afrika (CAF), ni kwamba kila nchi shiriki inatakiwa kuwa na wachezaji 23 kwenye michuano hiyo, ambapo kutokana na taratibu hizo Maximo amelazimika kuwaacha wachezaji wanne kati ya 27, alionao sasa.
  Hivyo wachwezaji watakaokwenda Ivory Coast ni Deogaratius Boniventure, Shaabani Dihile, Farouk Ramadhan, Erasto Nyoni, Shadrack Nsajigwa, Salum Sued, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Juma Jabu, Amir Maftah, Nurdin Bakari, Geoffrey Boniface, Henry Joseph, Shaaban Nditi, Haruna Moshi, Nizar Khalfani, Athumani Idd na Abdi Kassim, Kigi Makasi, Mussa Hassani Mgosi, Mrisho Ngasa, Jerry Tegete na Mwinyi Kazimoto.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAXIMO ATAJA KIKOSI CHA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top