• HABARI MPYA

  Ijumaa, Februari 20, 2009

  NDONDI, MAWE LUXURY PUB NDANI YA TMK

  na mohamed mharizo
  MABONDIA Sule Kato na Anthony Mwakapilila wanatarajia kupanda ulingoni Februari 28 mwaka huu katika pambano la ngumi za kulipwa lisilo la ubingwa la uzito wa Middle, raundi 6 litakalofanyika katika ukumbi wa Luxury Pub jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza jana Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania{TPBO},Yasin Abdallah alisema kuwa lengo la pambano hilo ni kupima viwango vya mabondia hao na kuboresha rekodi zao.
  Aidha alisema kuwa kutakuwepo mapambano ya utangulizi ambapo Salehe Salim wa Dar es Salaam atapambana na bondia Hussein Makrosi kutoka Iringa ambalo litakuwa la raundi 6 uzito wa Welter, wakati Juma Mkundi na Deo Samuel watapigana katika uzito wa Feather kwa raundi 4 na Haruna Mnyalukolo atazipiga na Ramadhan Kumbele kwa raundi 4 uzito wa kilo Super Bantam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDONDI, MAWE LUXURY PUB NDANI YA TMK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top