• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 02, 2009

  MISS EAST AFRICA JULAI 8 BUJUMBURA

  Rais wa zamani Burundi, Pierre Buyoya
  Miss East Africa, Claudia Niyonzima akiteta
  jambo na Waziri wa Afrika Mashariki (Burundi), Hafsa Mossi
  kwenye hafla ya uzinduzi wa shindano la mwaka huu.
  *****
  MASHINDANO ya Miss East Africa yatafanyika Julai 8, mwaka huu mjini Bujumbura, Burundi, ikiwa ni mara ya pili kufanyika nchini humo tangu yarejeshwe mwaka jana.
  Mashindano hayo yaliznduliwa Januari 31 mjini humo katika sherehe zilizohudhuriwa na watu mbalimbali mashuhuri, akiwemo rais mstaafu wa nchi hiyo ndugu Pierre Buyoya.
  Akitangaza rasmi tarehe ya kufanyika kwa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Rena Events Limited ya Dar es Salaam, ambao ndio waandaaji wa mashindano hayo, Eena Callist, alisema kwamba fainali za Miss East Africa mwaka huu zitafana zaidi.
  Kufanyika tena kwa mashindano hayo mjini Bujumbura, kunafuatia ombi la rais wa Burundi kwa waandaaji, Rena Events baada ya kuridhishwa na kiwango cha hali ya juu cha mashindano yaliyofanyika mwaka jana nchini humo.
  Katika mashindano ya mwaka jana, mrembo Claudia Niyonzima wa Burundi aliibuka mshindi wa mashindano hayo na kujinyakulia gari la kisasa aina ya Lexus RX 300 lenye thamani ya sh millioni 35.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MISS EAST AFRICA JULAI 8 BUJUMBURA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top