• HABARI MPYA

  Jumamosi, Februari 21, 2009

  KILA LA HERI TAIFA STARS...

  IKIWA na hasira za kipigo cha mabao 4-0 mjini Dakar, Senegal, mwaka juzi, timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo inashuka kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny mjini hapa kumenyana na Simba hao wa Teranga katika mchezo wa kwanza kabisa wa michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
  Stars ilifungwa na Senegal mabao hayo katika mchezo wa kundi la saba, kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka jana nchini Ghana, lakini ziliporudiana mjini Mwanza zilitoka sare ya 1-1, ingawa bao la Simba wa Teranga lililotiwa kimiani na Diomansy Kamara lilikuwa la utata.
  Stars iliyowasili mjini hapa Alhamisi mchana, ikifuatiwa na Simba hao wa Teranga waliotua jioni, wachezaji wake wapo katika hali nzuri na kwa pamoja na kocha wao Mbrazill, Marcio Maximo wameahidi kuifunga Senegal leo.
  Katika mchezo wa leo, Maximo anatarajiwa kuanza na kikosi chake cha kawaida, langoni akisimama Shaaban Dihile, beki wa kulia Nahodha Nsajigwa Shadrack, kushoto Juma Jabu, katikati Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Salum Sued, kiungo wa ulinzi Geoffrey Bonny, kiungo wa kulia Mrisho Ngassa, katikati Henry Joseph, kushoto Athumani Iddi na washambuliaji Haruna Moshi ‘Boban’ na Jerry Tegete.
  Kwenye benchi wanaweza kuwapo, Farouk Ramadhan, Amir Maftah, Nurdin Bakari, Mwinyi Kazimoto, Abdi Kassim, Kiggi Makasi na Mussa Hassan Mgosi.

  RATIBA KAMILI CHAN 2009:
  22/2/09

  Mechi muda mji
  1. Ivory Coast Vs Zambia (Saa 1:00 jioni) Abidjan
  2. Senegal Vs Tanzania (Saa 9:00 alasiri) Abidjan
  23/02/09
  3. Ghana Vs Zimbabwe (Saa 12:00 joni) Bouake
  4. DRC Vs Libya (Saa 10: 00 jioni) Bouake

  25/02/09
  5. Zambia Vs Senegal (saa 1:00 usiku) Abidjan
  6. Tanzania V I. Coast (Saa 9: alasiri) Abidjan

  26/02/09
  7. Zimbabwe Vs DRC (Saa 12: jioni) Bouake
  8. Libya Vs Ghana (saa 10: jioni) Bouake

  28/02/09
  9. Ivory Coast Vs Senegal (Saa 10:00 jioni) Abidjan
  10. Zambia Vs Tanzania (Saa 10:00 jioni) Bouake

  01/03/09
  11. Ghana Vs DRC (saa 10:00 jioni) Bouake
  12. Zimbabwe Vs Libya (Saa 10:00 jioni) Abidjan

  NUSU FAINALI:
  04.03.09
  13. Mshindi wa kwanza B Vs Mshindi wa Pili A (saa 9:00 Alasiri) Bouake
  14. Mshindi wa kwanza A Vs Mshindi wa Pili B (Saa 1:00 usiku) Abidjan

  KUTAFUTA MSHINDI WA TATU:
  7/03/09, Abidjan

  FAINALI:
  08/03/09, Abidjan
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILA LA HERI TAIFA STARS... Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top