• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 02, 2009

  MANJI AITEMA YANGA

  Enzi za furaha Manji na Yanga; Hapa akiwa na rais wa zamani wa klabu hiyo, Francis Kifukwe ambaye chini ya utawala wake ndio klabu hiyo ilimpata mfadhili huyo, aliyewafanyia makubwa wana Jangwani. Hakika hili ni pigo.

  YUSSUF Mehboob Manji si mfadhili tena wa klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, kwani vyanzo vya habari vimesema amejitoa rasmi baada ya kumaliza Mkataba wake wa miezi mitatu alioongeza.
  Imeelezwa Manji aliongeza Mkataba huo mfupi, baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kujitokeza kuidhamini klabu hiyo mwaka jana.
  Manji ambaye amekuwa akiisadia Yanga kwa mambo mengi katika kipindi chote ambacho aliingia mkataba, alianza kusitisha udhamini wake baada ya TBL kuingia mkataba wa kuifadhili klabu hiyo, katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na watani wao wa jadi, Simba.
  Lakini pamoja na kujitoa, Manji hajaitelekeza moja kwa moja klabu hiyo, kwani amekuwa akiwakopesha fedha viongozi wa klabu hiyo kwa ajili ya maandalizi ya shughuli mbalimbali za klabu na kuzirejesha kupitia mapato ya milangoni kwenye mechi zao.
  Hivyo ndivyo alivyofanya pia kwenye mechi dhidi ya Etoile d’Or Mirontsy ya Comoro, katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, uliofanyika Jumamosi iliyopita, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Siku hiyo, wafanyakazi wa Quality Group, kampuni inayomilikiwa na Manji walionekana wakisimamia mapato kwa ajili ya kusubiri kukata fedha za bosi wao, ili wazirejeshe.
  Kujitoa kwa Manji aliyeisaidia klabu hiyo kusajili kikosi cha nyota wenye thamani ya Sh. Milioni 500, kunafanya klabu hiyo ibakiwe na mdhamini mmoja tu, TBL.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MANJI AITEMA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top