• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 09, 2009

  AKUDO IMPACT KUPEKECHA MLANDIZI

  BENDI ya muziki wa dansi ya Akudo Impact 'Vijana wa Masuti', kesho watafanya onyesho la kwanza katika ukumbi wa Chemchem uliopo Mlandizi mkoani Pwani. Akizungumza na gazeti hili, Mratibu wa onesho hilo, Frank Nelson, alisema Akudo Impact watawapa mashabiki wa muziki maeneo hayo nyimbo zao mpya zilizomo kwenye albamu ya Impact ambayo inatamba hivi sasa.“Rais wa bendi Christian Bella ameahidi kukonga nyoyo za mashabiki wa muzikiukizingatia ni onesho maalum kwa wakazi wa maeneo hayo na jirani,” alisema.Onesho hilo maalum la kuelekea katika siku ya wapendanao limedhaminiwa na kampuni ya Bia ya Serengeti Limited na kuwataka mashabiki wa muziki kuhudhuria ili waweze kuona shoo maalum ya vijana hao.Mratibu huyo alisema kwamba, kiingilio katika onesho hilo kimepangwa kuwa sh. 5,000 kwa mtu mmoja ikiwa ni maalum kwa mashabiki ambao hawajawahi kuwashuhudia vijana hao wa masauti wakifanya vitu vyao jukwaani.Amezitaja nyimbo zitakazoimbwa jukwaani ni Mapenzi kitu gani, Binadamu, Mama Vanessa, Shukrani Muzamil, Safari siyo kifo na Papa Msofe.“Nyimbo ni nyingi na mashabiki wetu wataridhika wenyewe, kwanza wajue watapata vitu vya uhakika kuanzia shoo mpaka utamu wa sauti,” alisema.Ijumaa bendi hiyo itasafiri mpaka mkoani Morogoro ambako itafanya onesho maalum la mkesha wa Wapendao kwenye ukumbi wa Gronency mjini humo.Pia, Siku ya Wapendanao, bendi hiyo itarajea jijini Dar es Salaam na kufanya onyesho lao katika ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni jijini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: AKUDO IMPACT KUPEKECHA MLANDIZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top