• HABARI MPYA

  Jumatatu, Februari 02, 2009

  MAXIMO ATAJA JESHI OLA CHAN

  Maximo akizungumza na Waandishi wa Habari


  KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoshiriki michunao ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) nchini Ivory Coast, baadaye mwaka huu kimetajwa leo na kocha Marcio Macimo.
  Katika kikosi hicho, Maximo ambaye ni raia wa Brazil, Salvatory Ntebe, Erasto Nyoni wa Azam FC, Jabir Aziz wa Simba, Uhuru Suleiman wa Mtibwa Sugar, Mwinyi Kazimotowa JKT Ruvu, Zahoro Pazi (Mtibwa Sugar), Deogratius Munishi (Simba), Shaaban Dihile (JKT Ruvu), Farouk Ramadhan (Miembeni), Shadrack Nsajigwa (Yanga), Salum Sued (Mtibwa Sugar), Nadir Haroub ‘Canavaro (Yanga), Kelvin Yondan (Simba), Juma Jabu (Simba) , Amir Maftah (Yanga) na Nurdin Bakari (Yanga).
  Wengine ni Henry Joseph (Simba), Geoffrey Bonny (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar), Haruna Moshi (Simba), Nizar Khalfan (Moro United), Athumani Idd ‘Chuji’ (Yanga), Abdi Kassim (Yanga), Mussa Hassan ‘Mgosi’ (Simba), Jerson Tegete (Yanga), Mrisho Ngassa (Yanga) na Kigi Makasi (Yanga)].
  Stars inatarajiwa kuingia kambini kesho jioni kujiandaa na mchezo wa kujipima nguvu dhidi ya Zimbabwe, uliopangwa kufanyika Februari 11, mwaka huu.
  Katika fainali za CHAN zilizopangwa kuanza Februari 22, mwaka huu, Stars imepangwa katika kundi A pamoja na Senegal, Zambia na wenyeji Ivory Coast, wakati kundi B linaundwa na Ghana, Zimbabwe, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) na Libya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAXIMO ATAJA JESHI OLA CHAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top