• HABARI MPYA

    Sunday, August 13, 2017

    OKWI AING’ARISHA SIMBA TAIFA, YAIPIGA MTIBWA 1-0

    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    SIMBA SC imeendeleza wimbi la ushindi katika mechi za kujipima nguvu baada ya kuichapa 1-0 Mtibwa Sugar ya Morogoro jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Huo ni ushindi wa pili mfululizo kwa timu ya kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog baada ya Jumanne kuwalaza 1-0 mabingwa wa Ligi ya Azam Rwanda, Rayon Sport hapo hapo Taifa.  
    Katika mchezo wa leo, Mtibwa Sugar ilipata pigo dakika ya 30 baada ya kipa wake namba moja, Shaaban Hassan Kado kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na maumivu ya goti kufuatia kugongana na mshambuliaji wa Simba, John Raphael Bocco.
    Mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi (kulia) akishangilia baada ya kuifungia Simba bao pekee leo. Kushoto ni Shiza Kichuya
    Emmanuel Okwi akimtoka akimtoka beki wa Mtibwa Sugar, Hassan Isihaka
    Mshambuliaji wa Simba, John Bocco akipiga kichwa dhidi ya beki wa Mtibwa
    Kiungo wa Simba, Haruna Niyonzima akimtoka kiungo wa Mtibwa Mohammed Issa 'Banka'

    Kipa wa pili, Abdallah Makangana akaenda kuchukua na nafasi na dakika ya 44 Simba SC wakapata bao kupitia kwa mshambuliaji wake nyota, Mganda Emmanuel Okwi aliyemalizia pasi ya mshambuliaji mpya, Bocco aliyesajiliwa kutoka Azam FC.
    Kipindi cha pili, Simba SC iliendelea kung’ara uwanjani ikiongozwa na wachezaji wake nyota kama Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, Mganda Emmanuel Okwi na wazawa Sjiza Kichuya na John Bocco.
    Hata hivyo, pamoja na kutengeneza nafasi nyingi, kucheza mpira mzuri uliowasisimua mashabiki wake, Simba SC ilishindwa kuongeza bao.
    Baada ua mchezo huo, mapema kesho Simba inapanda boti kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Yanga SC Jumamosi Uwanja wa Taifa. 
    Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa;Said Mohammed, Ally Shomary, Jamal Mwambeleko/Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ dk46, Salim Mbonde, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya/Said Ndemla dk67, Haruna Niyonzima, Muzamil Yassin/Laudit Mavugo dk86, John Bocco/Jonas Mkude dk86 na Emmanuel Okwi.
    Mtibwa Sugar; Shaaban Kado/Abdallah Makangana dk30, Salum Kanoni, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Hassan Isihaka, Dickson Job, Shaaban Nditi, Ally Makarani, Mohammed Issa, Hussein Javu, Salehe Hamisi/Kelvin Sabato dk64 na Salum Ramadhani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: OKWI AING’ARISHA SIMBA TAIFA, YAIPIGA MTIBWA 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top