• HABARI MPYA

    Friday, August 18, 2017

    BARCA, REAL WAOMBOLEZA VIFO VYA MASHAMBULIO YA KIGAIDI

    WACHEZAJI wa Barcelona na benchi lao la Ufundi, leo walilazimika kusimama kimya kwa dakika moja kabla ya mazoezi yao ili kuwafariji watu waliokufa katika milipuko ya kigaidi mjini humo.
    Mashambulio mawili ya gari mjini Barcelona nja ukanda ewa bahari mjini Cambrils Alhamisi na mapema Ijumaa asubuhi yamechukua uhai wa watu 14, huku wengine wapatao 130 wakijeruhiwa. 
    Polisi wamewapiga risasi na kuwaua watu watano waliojivalisha mabomu feki baada ya shambulio la Cambrils, wakati dereva wa basi dogo lililotumika kwenye shambulio la Barcelona bado hajapatikana. 

    Wachezaji wa Barcelona na makocha wao wakiwa kimya leo kabla ya mazoezi yao PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

    Mapema tu Barca ilithibitisha wachezaji wake watafunga vitambaa vyeusi mikononi kwenye mchezo wao wa ufunguzi wa msimu mpya wa La Liga dhidi ya Real Betis Uwanja wa Nou Camp Jumapili.
    Real Madrid nao walitulia kwa dakika moja kabla ya kuanza mazoezi ya Ijumaa, kufuatia mashambulio mawili ya kigaidi nchini Hispania.
    Real wanatarajiwa kuanza kampeni ya kutetea taji lao Ligi Kuu ya Hispania, maarufu kama La Liga ugenini dhidi ya Deportivo La Coruna Jumapili
    Wakati huo huo: Kocha wa zamani wa Barcelona, Pep Guardiola ambaye kwa sasa anafundisha 
    Manchester City naye ametoa pole kwa tukio hilo.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BARCA, REAL WAOMBOLEZA VIFO VYA MASHAMBULIO YA KIGAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top