• HABARI MPYA

  Monday, August 07, 2017

  SNEIJDER ATUA NICE KUMPIKIA MABAO BALOTELLI

  KIUNGO mkongwe, Wesley Sneijder ameungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa Inter Milan, Mario Balotelli baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Nice ya Ufaransa kama mchezaji huru.
  Mwanasoka huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, mwenye umri wa miaka 33 sasa, ameondoka Galatasaray majira haya baada ya misimu minne ya kufanya kazi Uturuki.
  Nice imesema jana kwamba; "Tumefikia makubaliano Jumapili hii baina yetu OGC Nice na Wesley Sneijder!'
  Na leo mchana wametangaza kwamba mchezaji huyo amesaini mkataba, ambao unaweza kufutwa iwapo hatafuzu vipimo vya afya. 
  Wesley Sneijder ameungana na Mario Balotelli baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na Nice ya Ufaransa PICHA ZAIDI GONGA HAPA  
  Kiungo huyo mshambuliaji amesaini mkataba wa mwaka mmoja na timu ya Lucian Favre, ambayo ilifungwa 1-0 na Saint-Etienne katika mechi ya ufunguzi ya Ligi ya Ufaransa msimu huu.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SNEIJDER ATUA NICE KUMPIKIA MABAO BALOTELLI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top