• HABARI MPYA

  Monday, August 07, 2017

  NIYONZIMA: MIMI SASA NI SIMBA, KARIBUNI TAIFA KESHO

  Na Rehema Lucas, DAR ES SALAAM
  KIUNGO mpya wa Simba, Haruna Hakizimana Fadhili Niyonzima amesema kwamba ataacha kazi yake iongee uwanjani baada ya kusaini mkataba wa kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.
  Akizungumza katika hafla maalum ya kutambulishwa kwake leo makao makuu ya klabu, Msimbazi, Dar es Salaam, Niyonzima amesema kwamba hatapenda kuzungumza mengi, bali watu waje wapne vitu vyake uwanjani kesho.
  Haruna anatarajiwa kuichezea Simba kwa mara ya kwanza kesho Uwanja wa Taifa, Dar e Salaam katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Rayon Sport ya kwao, Rwanda kufutia kujiunga na Wekundu hao wa Msimbazi kama mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake mahasimu wa jadi, Yanga.
  Hajji Manara akimtambulisha Haruna Niyonzima leo makao makuu ya Simba, Msimbazi, Dar es Salaam
  Hajji Manara akimtambulisha Nicholas Gyan leo makao makuu ya Simba, Msimbazi, Dar es Salaam 
  Emmanuel Okwi alifanya mazoezi asubuhi ya leo Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam

  “Ninamshukuru Mungu nimefika salama Tanzania, mimi kwa sasa ni mchezaji halali wa Simba, sina mengi ya kuongea, tukutane uwanjani kesho,”amesema Haruna aliyedumu kwa miaka sita Yanga baada ya kujiunga nayo mwaka 2011 akitokea APR ya kwao, Rwanda.
  Mchezo wa kesho unaohitimisha kilele cha wiki ya Simba na tamasha la Simba Day, ni maalum kwa klabu hiyo kutambulisha kikosi chake cha msimu mpya ambao na umekuwa utamaduni wa klabu hiyo kwa miaka saba sasa.
  Katika mkutano wa leo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Hajji Sunday Manara alisema mgeni rasmi wa kesho atakuwa Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais, Januari Makamba.
  Mbali na Niyonzima, wachezaji wengine wapya waliotambulishwa leo Simba SC ni pamoja na Mganda, Emmanuel Okwi anayerejea tena Msimbazi na mshambuliaji Mghana, Nicholas Agyei. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NIYONZIMA: MIMI SASA NI SIMBA, KARIBUNI TAIFA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top