• HABARI MPYA

  Saturday, August 05, 2017

  CRISTIANO RONALDO ETI AMESEMA ANATAKA KURUDI ENGLAND

  MSHAMBULIAJI Cristiano Ronaldo amesema anataka kuondoka Real Madrid na kurejea England, sikua chache tu kabla ya kumenyana na timu yake, Manchester United katika mechi ya UEFA Super Cup.
  Radio Cadena Ser ya Hispania imesema kwamba Ronaldo aliyasema katika mazungumzo yake na Jaji nje ya Mahakama ya Madrid katika mfulululizo wa uchunguzi wa kesi yake kukwepa kodi kiais cha Euro14.7.
  Mchezaji huyo alikuwa ana mazungumzo binafsi na Jaji Monica Gomez Ferrer Jumatatu wiki hii ambayo si kawaida kuvuja kwenye kwenye vyombo vya Habari kama si kutolewa na wahusika wenyewe.
  Cristiano Ronaldo anataka kurejea England ambako hajawahi kupata matatizo ya kodi

  Cadena Ser iliripoti Ijumaa kwamba Ronaldo alimuambia Jaji: "Sijawahi kupata matatizo ya kodi England…ndiyo maana ningependa kurudi England,".
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CRISTIANO RONALDO ETI AMESEMA ANATAKA KURUDI ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top