• HABARI MPYA

  Saturday, August 05, 2017

  NAYMAR AZUIWA KUANZA KUCHEZA LIGUE 1 UFARANSA LEL

  MSHAMBULIAJI mpya wa Paris Saint-Germain, Neymar hataweza kuichezea timu hiyo leo katika mchezo wa ufunguzi wa Ligue 1 kutokana na usajili wake kutokamilika.
  PSG ilimtambulisha mwanasoka huyo ghali duniani kwenye vyombo vya Habari jana baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 200 kutoka Barcelona. 
  Neymar aliweka wazi mbele ya umati wa watu kwamba alikuwa tayari kucheza wa Uwanja Parc De Princes dhidi ya Amiens kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Ufaransa. 
  Pamoja na hayo, taarifa nchini Ufaransa zinasema kwamba bodi ya soka nchini humo (LFP), ilikuwa haijapata risiti ya uhamisho wa kimataifa hadi usiku wa jana ili kumsajili Neymar aweze kucheza leo mchana.

  Neymar (katikati) akiwa na wachezaji wenzake, Wabrazil Dani Alves (kushoto) na Lucas Moura mazoezini PSG jana PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  La Liga wamekuwa wakilalamikia sana uhamisho huo siku za karibuni hadi Rais wake, Javier Tebas akasema watafungua mashitaka Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kupinga matumizi mabaya ya fedha yaliyofanyika kumuhamishia Neymar Ligue 1 kutoka Hispania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NAYMAR AZUIWA KUANZA KUCHEZA LIGUE 1 UFARANSA LEL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top