// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); REFA AMPUNGUZIA MABAO BOCCO, LAKINI BADO YUPO MATAWI YA JUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE REFA AMPUNGUZIA MABAO BOCCO, LAKINI BADO YUPO MATAWI YA JUU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, December 04, 2012

    REFA AMPUNGUZIA MABAO BOCCO, LAKINI BADO YUPO MATAWI YA JUU

    Bocco akiwawajibisha mabeki wa Rwanda juana

    Na Mahmoud Zubeiry, Kampala
    KAMA si refa kukataa bao lake safi tu alilofunga katika mechi ya Kundi B dhidi ya Burundi, leo Bocco angekuwa kileleni kwenye msimamo wa wafungaji wa mabao katika Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge kwa mabao sita, lakini kufanyiwa dhuluma hiyo ana mabao matano.
    Hata hivyo, jambo moja tu ameonyesha Bocco mjini hapa, yeye ni mfungaji wa uhakika anapocheza kwenye mazingira mazuri pasipo kuzomewa zomewa na mashabiki anapokosea kidogo kibinadamu.
    Hiyo inatokana na Bocco kufunga katika mechi aliyocheza kuanzia hatua ya makundi, dhidi ya Sudan mabao mawili, Burundi moja lililokataliwa, Somalia mawili na jana mojas dhidi ya Rwanda.
    Bocco sasa ina idadi sawa ya mabao na Mrisho Ngassa wa Tanzania Bara pia, ambaye yeye alifunga mabao yote katika mechi moja dhidi ya vibonde Somalia.
    Bocco na Ngassa wanafuatiwa kwa mbali na Brian Umony wa Uganda mwenye mabao matatu, sawa na Warundi wawili, Suleiman Ndikumana na Christopher Nduwarugira katika mbio za kiatu cha dhahabu cha mashindano haya.
    Khamis Mcha ‘Vialli’ wa Zanzibar, David Ochieng, Clifton Miheso wote wa Kenya na Dadi Birori au Taddy Etikiama wa Rwanda, wote wana mabao mawili kila mmoja.

    WAFUNGAJI CECAFA TUSKER CHALLENGE 2012
    John Bocco                     Tanzania 5
    Mrisho Ngassa               Tanzania 5
    Brian Umony                  Uganda    3
    Suleiman Ndikumana Burundi   3 (1 penalti)
    Chris Nduwarugira        Burundi   3
    Khamis Mcha                 Zanzibar  2
    David Ochieng               Kenya       2
    Clifton Miheso               Kenya       2
    Dadi Birori                      Rwanda   2
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: REFA AMPUNGUZIA MABAO BOCCO, LAKINI BADO YUPO MATAWI YA JUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top