• HABARI MPYA

  Ijumaa, Desemba 21, 2012

  UMONY AOMBA UDHURU AZAM

  Umony

  Na Mahmoud Zubeiry, Kinshasa
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Brian Umony atajiunga na klabu yake mpya, Azam FC baada ya sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya, imeelezwa.
  Katibu wa Azam FC, Nassor Idrisa ameiambia BIN ZUBEIRY mjini hapa kwamba, Umony ameomba aje kuanza kazi baada ya sikukuu na uongozi umemkubalia.
  Azam inatarajiwa kuondoka hapa mapema Jumatatu kurejea Dar es Salaam baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Hisani mjini hapa Jumapili.
  Nassor amesema timu ikirejea Dar es Salaam wachezaji watapewa mapumziko ya siku mbili kwa ajili ya sikukuu na baada ya hapo, watarudi kambini tayari kwa safari ya Zanzibar kwenye Kombe la Mapinduzi.
  Azam ambao ndio mabingwa watetezi wa Kombe la Mapinduzi, leo watacheza mechi ya Nusu Fainali na Shark FC Uwanja wa Martyrs na Jumapili watacheza mechi ya mwisho, iwe ya kusaka mshindi wa tatu au ubingwa, itategemea na matokeo ya leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: UMONY AOMBA UDHURU AZAM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top