• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 30, 2012

  YANGA WABADILI HOTELI ANTALYA, KIKOSI CHAFIKA SALAMA TAYARI KWA MAFUNZO  Wachezaji wa Yanga wakiwa wamepumzika katika Uwanja wa ndege wa kimataifa Instambul wakisubiria ndege ya kwenda katika mji wa Antalya
  Kikosi cha mabingwa wa kombe la Kagame mara mbili mfululizo timu ya Young Africans imewasili salama katika mji wa Antalya kusini mwa nchi ya Uturuki majira ya saaa 10:30 jioni   kwa saa za afrika mashariki na kati na moja kwa moja kupolekewa na wenyeji wake kampuni ya Team Travel.
  Young Africans imefikia katika hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika uwanja wa ndege wa antalya, ambapo hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya mediteranian.
  Mwanzoni Yanga ilikuwa ifikie katika hotel ya Sueno Beach Hotel iliyopo kilometa 70 kutoka uwanja wa ndege lakini jana siku moja kabla ya safari ilifanya mabadiliko na kuamua kuhamia katika hotel ya Fame Residence.
  Wachezaji wamefurahi mandhari ya hotel kwani ni miongoni mwa hotel za nyota tano katika mjii huu wa Antalya hivyo wamefariijika na kuupa hongera uongozi kwa hatua waliyofikia ya kukubaliana na mwalimu kuweka kambi ya mafunzo  nchini Uturuki.
  Timu itaanza mazoezi kesho asubuhi katika viwanja vilivyopo katika eneo la hotel ya fame, ambapo kwa siku timu itakua inafanya mazoezi mara mbili kwa siku asubuhi na jioni.
  Kuhusu hali ya hewa ni baridi kiasi na sio baridi kali kama ilivyokuwa inatangazwa na vyombo vya habari hapo awali.
  Mtandao wa klabu www.youngafricans.co.tz utaendelea kuwajuza juu ya kila kitu kinachojiri nchini Uturuki. 

  IMEHAMISHWA KUTOKA TOVUTI YA YANGA
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: YANGA WABADILI HOTELI ANTALYA, KIKOSI CHAFIKA SALAMA TAYARI KWA MAFUNZO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top