• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 20, 2012

  TFF YAWAPONGEZA ZEN C NA WENZAKE TWFA


  Na Princess Asia
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) linaupongeza uongozi mpya wa Chama cha Mpira wa Miguu wa Wanawake Tanzania (TWFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Desemba 19 mwaka huu) hoteli ya Midlands mjini Morogoro.
  Ushindi aliopata Lina Kessy aliyechaguliwa tena kuwa Mwenyekiti pamoja na wajumbe wengine wa Kamati ya Utendaji unaonesha jinsi ambavyo wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TWFA walivyo na imani kwao.
  TFF inaahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TWFA, na kwamba ina changamoto kubwa ya kuhakikisha inaendesha shughuli za chama hicho kwa kuzingatia katiba na kanuni.
  Pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA chini ya Mama Ombeni Zavala na Kamati ya Uchaguzi ya TFF inayoongozwa na Deogratias Lyatto kwa kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa utulivu na kwa kuzingatia Katiba ya TWFA na Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
  Safu mpya ya uongozi wa DRFA inaundwa na Lina Kessy (Mwenyekiti), Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti), Amina Karuma (Katibu), Zena Chande (Mwakilishi wa Mkutano Mkuu wa TFF) wakati mjumbe wa Kamati ya Utendaji ni Triphonia Temba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TFF YAWAPONGEZA ZEN C NA WENZAKE TWFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top