• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 30, 2012

  WAKENYA WA AZAM WATUA, UMONY KESHO CHAMAZI

  Atudo

  Na Prince Akbar
  BEKI Joackins Atudo na kiungo Humphrey Mieno wote raia wa Kenya, wamewasili jana Dar es Salaam kujiunga na klabu yao, Azam FC baada ya kumaliza kula sikukuu ya Krisimasi na keshokutwa watakuwapo kwenye kikosi kitakachokwenda visiwani Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
  Meneja Msaidizi wa Azam, Jemedari Said ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, mbali na wachezaji hao wa Kenya, mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Brian Umony atatua kesho.   
  Atudo na Mieno walikuwepo kwenye kikosi cha Azam kilichotwaa Kombe la Hisani la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), linaloandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la DRC wiki iliyopita, baada ya kuwachapa wenyeji, Dragons FC kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90.
  Azam iliingia fainali, baada ya kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya DRC Ijumaa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs.
  Kikosi kizima cha Azam kilichoshiriki mashindano hayo ni Kipre Tchetche, Seif Abdallah, Kipre Balou, Zahor Pazi, Jackson Wandwi, Malika Ndeule, Uhuru Suleiman, Omar Mtaki, Jabir Aziz, Ibrahim Mwaipopo, Gaudence Mwaikimba, Abdi Kassim, Luckson Kakolaki, Samih Hajji Nuhu, Mwadini Ally, Himid Mao, David Mwantika, Waziri Salum, Humphrey Mieno na Joackins Atudo.
  Katika mashindano hayo, Gaudence Mwaikimba aliibuka mfungaji bora kwa mabao yake matatu, ukiachilia mbali mawili ya penalti. Mchezaji mwingine wa kigeni wa Azam, Brian Umony wa Uganda, atajiunga na timu hiyo baada ya sikukuu pia.
  Azam wamepangwa Kundi B, katika Kombe la Mapinduzi pamoja na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
  Kundi A lina timu za Simba SC, Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba.
  Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WAKENYA WA AZAM WATUA, UMONY KESHO CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top