• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 27, 2012

  UBINAFSI UNAVYOHATARISHA NAFASI YA MSUVA UWANJANI

  Kiungo mshambuliaji chipukizi wa Yanga, Simon Msuva anatakiwa kubadilika kwa kuachana na kucheza soka ya kibinafsi na badala yake kucheza kwa maslahi ya timu, Msuva amekuwa akicheza kama yupo peke yake uwanjani, hawaangalii wenzake wapo katika nafasi gani ili aweze kuwapatia mipira. Anaweza akapewa mpira kwenye njia akachomoka nao vizuri, lakini akikaribia kwenye eneo la hatari, atataka kulazimisha kufunga mwenyewe hata kama hayuko kwenye nafasi nzuri, dhahiri desturi hiyo, imemfanya kocha wa timu ya taifa, Mdenmark Kim Poulsen sasa aanze kmumsahau benchi. Kim alianza kumpiga benchi winga huyo katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge nchini Uganda mwezi huu, lakini bado inaonekana kijana huyo hajapata fundisho lolote, kwani ameendelea na desturi hiyo. Katika mchezo wa kirafiki wa timu yake, Yanga dhidi ya Tusker jana Msuva alichangia kuikosesha timu yake ushindi kwa uchoyo wake. Alishindwa kumpa pasi mara mbili Jerry Tegete akiwa kwenye nafasi nzuri. Hii imanaanisha, Kocha wa Yanga, Mholanzi Ernie Brandts atakapochoshwa na desturi yake hiyo, anaweza kuamua kuanza kumuweka benchi na huo ukawa mwanzo wake wa kupotea kwenye ramani ya soka baada ya muda mfupi tangu aibuke. Ipo haja ya Msuva (pichani) kubadilika. Ni mchezaji mzuri, ana kasi, uwezo wa kumiliki mpira na kipaji, lakini ubinafsi unahatarisha nafasi yake uwanjani.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: UBINAFSI UNAVYOHATARISHA NAFASI YA MSUVA UWANJANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top