• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 22, 2012

  ARTETA AIPA USHINDI ARSENAL


   22 Disemba, 2012 - Saa 18:06 GMT
  Mikel Arteta
  Mikel Arteta akishangilia bao lake
  Mikel Arteta, aliifungia Arsenal bao la pekee na la ushindi wakati wa mechi yao ya leo dhidi ya Wigan.
  Ushindi huo ni wa tatu mfululizo kwa Arsenal tangu mwezi mwaka huu.
  Arouna Kone alipoteza nafasi nzuri ya kuifungia Wigan wakati wa mechi hiyo wakati alipokuwa ndani ya mstatili ya kupiga mkwaju ambao ulipaa juu ya mlingoti.
  Arteta alifunga bao hilo kupitia mkwaju wa penlti baada ya Jean Beausejour kumfanyia madhambi Theo Walcott.
  Wigan sasa imepoteza mechi yake sita kati ya nane za ligi kuu na imesalia mkiani kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier kwa mwaka wa tatu mfululizo.
  Katika mechi nyingine Gareth Barry alifunga bao kunako dakika ya 92 na kusaida Manchester City kuandikisha ushindi finyu didi ya Reading.

  Matokeo zaidi

  Sergio Aquero
  Sergio Aquero
  Kufuatia ushundi huo Manchester City imasalia katika nafasi ya pili alama tatu nyumba ya Manchester United ambayo inachuana na Swansea hiyo kesho.
  Newcastle nayo ilijizolea alama tatu muhimu pale ilipoilza Queens Park Rangers kwa bao moja kwa bila.
  Shola Ameobi ndiye aliyeifungia Newcastle bao lake ya ushindi ambao pia ni bao lake la kwanza msimu huu.
  Steven Fletcher alifunga bao lake na nane msimu huu na kuisadia timu ya Sunderland kuilaza Southampton kwa bao moja kwa bila.
  Hatten Ben Afra
  Hatten Ben Afra
  Ushindi huo sasa umeinusuru Sunderland kutokana na tishio la kuwa miongoni mwa timu ambazo huenda zikashushwa daraja.
  Tottenham imetoka sare ya kutofungana bao lolote la Stoke City kati mechi ya kusisimua iliyochezwa katika uwanja wa White Hart Lane.
  Kufuatia sare hiyo Stoke, sasa imecheza mechi nane bila kupoteza na nusuru ifunga bao kunako dakika ya kwanza, lakini mkwaju wa Kenwyne Jones ulipaa juu ya mlingoti.
  West Brom nayo imesitisha rekodi ya Norwich ya kutoshindwa pale ilipoilaza kwa magoli mawili kwa moja.
  Everton ikatoka nyuma ya kufungwa bao moja na kushinda kwa magoli mawili kw moja dhidi ya West Ham United.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ARTETA AIPA USHINDI ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top