• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 23, 2012

  MWAIKIMBA ABEBA KIATU CHA DHAHABU DRC

  Gaudence Mwaikimba; Mfungaji bora Kombe la Hisani DRC

  Na Mahmoud Zubeiry, Kinshasa
  MSHAMBULIAJI Gaudence Mwaikimba wa Azam amekuwa mfungaji wa mashindano ya Kombe la Hisani yaliyoandaliwa na FECOFA, Shirikisho la Soka la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) baada ya kumaliza na mabao matatu, akifuatiwa na Kipre Herman Tchetche na Ngulubi Kilua wa Shark FC waliofunga mawili kila mmoja.
  Jumla pamoja na penalti za baada ya dakika 90 za mechi, Mwaikimba amefunga mabao matano, Kilua matatu na Kipre matatu.
  Hata hivyo, kwa kuwa mashindano haya ni ya hisani, hakutakuwa na zawadi mwa bingwa wala wachezaji bora, hivyo Mwaikimba anaondoka DRC na hadhi tu ya ufungaji bora.  
  Azam jana iliwafunga wenyeji Dragons FC kwa penalti 4-2, kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs mjini hapa na kutwaa Kombe. Azam walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 12 kabla ya Dragons kusawazisha dakika ya 75.
  Katika mikwaju ya penalti, kipa Mwadini Ally alicheza mikwaju miwili ya Dragons, wakati Gaudence Mwaikimba, Himid Mao, Joackins Atudo na Samih Hajji Nuhu walifunga penalti za Azam.
  Hata hivyo, Azam jana hawakukabidhiwa Kombe uwanjani hapo baada ya waandaji kusema wanakwenda kulipamba kwanza, hivyo sherehe za makabidhiano ya Kombe zinaweza kufanyika leo.
  Azam iliingia fainali, baada ya juzi kufanikiwa kuitoa kwa mikwaju ya penalti 5-4 Shark FC ya hapa, kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 90 kwenye Uwanja wa Martyrs. Azam inatarajiwa kuondoka hapa kesho mchana kurejea Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MWAIKIMBA ABEBA KIATU CHA DHAHABU DRC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top