• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 30, 2012

  BASIHAYA STARS WATWAA KOMBE LA MAJISAFI

  Diwani wa Kata ya Boko, Sharrif Majisafi (kushoto) akimkabidhi Kombe Nahodha wa Basihaya, Akilimali Bashir jioni hii kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Boko 

  Na Mahmoud Zubeiry
  TIMU ya Basihaya Stars leo imeibuka bingwa wa michuano ya Kombe la Diwani Sharrif Majisafi baada ya kuifunga Bunju Stars mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Boko, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, timu hiyo imezawadiwa pikipiki yenye thamani ya Sh. Milioni 1.9, seti ya jezi yenye thmani ya Sh. 300,000, Kombe na mpira, wakati washindi wa pili walipata seti ya jezi ya thamani ya Sh. 200,000, Kombe na mpira na mshindi wa tatu, Boko Kati alipata seti ya jezi ya Sh, 200,000, Kombe na mpira.
  Katika mchezo huo, dakika 45 za kipindi cha kwanza zilimalizika bila nyavu kutikisika na kipindi cha pili ndipo Basihaya waliokuwa wakicheza ‘barazani kwao’ walipochangamkia nyavu.
  Shujaa wa timu hiyo inayoundwa na vijana wengi chini ya umri wa miaka 20, alikuwa Shaaban Abesh aliyefunga mabao yote hayo katika dakika za 64 na 77.
  Bunju ilizinduka baada ya kufungwa mabao hayo ya ‘chap chap’ na kushambulia kwa nguvu langoni mwa wapinzani wao, lakini bahati haikuwa yao.
  Mgeni rasmi na mwandaaji wa mashindano, Diwani Majisafi alikabidhi Kombe kwa bingwa na fedha, wakati waalikwa wengine, Mama Janet Rite, Diwani wa Kata ya Kunduchi alikabidhi kwa washindi wa tatu, Ofisa Utamaduni wa Manispaa ya Kinondoni, Jumanne Mrimi alikabidhi zawadi za washindi wa pili.
  Dullah Carlos aliyeibuka mfungaji bora kwa mabao yake sita, alizawadiwa mpira.
  Mechi hiyo ilivutia mamia ya wakazi wa Boko na meneo jirani na kwa ujumla uwanja wa ulipendeza kutokana na idadi kubwa ya akina mama, baba na watoto waliojitokeza.
  Vimbwanga vya aina mbalimbali vya mashabiki vilikuwa sehemu ya burudani kwenye Uwanja huo, wengine walilewa chakari hadi kumwaga bia mithili ya shampeni wakati wakishangilia na kali zaidi ni njemba iliyoibuka na ngedere. Upadne wa vyoo vya shule, ilikuwa ni mioshi na harufu ya bangi tu ya masela waliokuwa wakifuatilia mechi kwa mbaaali. Ilikuwa burudani. 
  Kipute

  Zawadi ya pikipiki inatolewa

  Cheki watoto

  Pati la ubingwa

  Mabingwa

  Kuumia huku halafu hakuna ushindi, mchezaji wa Bunju

  Mchizi na ngedere wake

  Mama Zero anamwaga bia kwa furaha

  Mama Zero na patna wake wanamwaga bia kwa raha zao

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BASIHAYA STARS WATWAA KOMBE LA MAJISAFI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top