• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 20, 2012

  TENGA ATOA NOTISI KWA MUJIBU WA KATIBA

  Tenga

  Na Prince Akbar
  RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ambaye ndiye Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho hilo tayari ametoa notisi ya mkutano huo utakaofanyika Februari 23 na 24 mwakani jijini Dar es Salaam.
  Mkutano huo utafanyika Februari 23 mwakani na kufuatiwa na ajenda ya uchaguzi siku inayofuata. Ajenda ya uchaguzi iko chini ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
  Notisi hiyo imetumwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao ni kutoka vyama vya mpira wa miguu vya mikoa, vyama shiriki, klabu za Ligi Kuu ya Vodacom na wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF.
  Ajenda za Mkutano Mkuu zitatumwa kwa wajumbe siku 15 kabla ya mkutano huo wenye wajumbe zaidi ya 100.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: TENGA ATOA NOTISI KWA MUJIBU WA KATIBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top