• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 23, 2012

  MCHEZAJI COASTAL UNION AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO TANGA

  Boniface Wambura,
  Ofisa Habari TFF

  Na Princess Asia
  SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Coastal Union, Mussa Rico kilichotokea jana (Desemba  22 mwaka huu) jijini Tanga.
  Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba, msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti akiwa mchezaji Rico, na baadaye kocha alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea na kufundisha ikiwemo Coastal Union, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
  Amesema TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Rico, Chama cha Soka Tanga (TRFA) na klabu ya Coastal Union na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
  Amesema mazishi yanatarajiwa kufanyika leo (Desemba 23 mwaka huu) mkoani Tanga. Mungu aiweke roho ya marehemu Rico mahali pema peponi. Amina
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MCHEZAJI COASTAL UNION AFARIKI DUNIA, KUZIKWA LEO TANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top