• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 26, 2012

  BRANDTS AIONGOZA YANGA KATIKA MECHI YA 10 LEO

  Brandts; Kuiongoza Yanga katika mechi ya 10 leo

  Na Mahmoud Zubeiry
  YANGA SC ya Dar es Salaam, leo itamenyana na mabingwa wa Kenya, Tusker FC katika mchezo wa kirafiki utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Huo utakuwa mchezo wa 10 kwa ujumla, Yanga kucheza chini ya kocha wake mpya, Mholanzi Ernie Brandts kati ya hiyo, ikishinda saba, sare moja na kufungwa moja.
  Brandts aliyerithi mikoba ya Mbelgiji Tom Saintfiet, amekuwa akiinoa timu hiyo kwa takriban wiki tatu sasa kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu pamoja na Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
  Mabingwa hao wa Kagame, mwishoni mwa wiki hii wanatarajiwa kufanya ziara ya wiki mbili nchini Uturuki, kujiandaa na kampeni zake za mwakani. Yanga itaondoka na kikosi chake chote na hakuna mchezaji atakayeachwa.   

  REKODI YA ERNIE BRANDTS YANGA
  Yanga 1-1 Simba SC            (Ligi Kuu)
  Yanga 0-1 Kagera Sugar    (Ligi Kuu)
  Yanga 3-1 Toto African      (Ligi Kuu)
  Yanga 3-2 Ruvu Shooting  (Ligi Kuu)
  Yanga 3-0 Polisi Moro       (Ligi Kuu)
  Yanga 1-0 JKT Oljoro          (Ligi Kuu)
  Yanga 3-0 JKT Mgambo     (Ligi Kuu)
  Yanga 2-0 Azam FC             (Ligi Kuu)
  Yanga 2-0 Coastal               (Ligi Kuu)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BRANDTS AIONGOZA YANGA KATIKA MECHI YA 10 LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top