• HABARI MPYA

    Thursday, December 27, 2012

    SIMBA SC YAPANGWA NA TUSKER FC YA KENYA MAPINDUZI CUP

    Simba SC

    Na Ally Mohamed, Zanzibar
    MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba SC wamepangwa kundi moja, A na Tusker FC ya Kenya, Bandari ya Unguja na Jamhuri ya Pemba katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni visiwani Zanzibar.
    Aidha, katika Kundi B, washindi wa pili wa Ligi Kuu ya Bara, Azam FC ya Dar e Salaam pia, imepangwa na Mtibwa Sugar ya Morogoro, Coastal Union  ya Tanga na Miembeni ya Unguja.
    Michuano ya Kombe la Mapinduzi, ambayo ni maalum kwa ajili ya kuherehekea Mapinduzi matukufu ya Zanzaibar, inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 2, hadi kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Januari 12, mwakani, huku ikishirikisha timu kutoka ndani na nje ya Tanzania.
    Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo iliyotolewa na Kamati Maalum ya Kusimamaia michuano hiyo, inaonesha kuwa katika mchezo wa kwanza utakaochezwa siku ya ufunguzi itakuwa ni kati ya Bandari kutoka Unguja ambayo itacheza na Jamhuri kutoka kisiwani Pemba ambao ni wawakilishi wa Zanzibar katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika, pamabano litakalochezwa katika uwanja wa Mao Tse Tung mjini Unguja, huku usiku wa siku hiyo hiyo katika Uwanja wa Amaan kisiwani Unguja pambano la ufunguzi rasmi katika mashindano hayo likiwakutanisha mabingwa wa soka nchini Tanzania, Simba SC ambao watapambana na mabingwa wa soka nchini Kenya, Tusker.
    Kwa mujibu wa ratiba hiyo jumla ya timu nane zitashiriki katika mashindano hayo ambayo yamejipatia umaarufu mkubwa visiwani hapa, timu hizo zimegawanya katika makundi mawili ambayo ni kama ifuatavyo:
    Awali michuano hiyo ilitarajiwa kuanza kisiwani Pemba tarehe 1 Januari, lakini kutokana na kujitoa katika mashindano kwa klabu ya Al-Ahly ya Misri kutokana na klie kilichoelezwa sababu za kiusalama, mechi zote sasa zitachezwa kisiwani Unguja na ufunguzi ukipangwa kuanza tarehe 2 badala ya tarehe 1 januari.
    Bingwa wa michuano hiyo ataondoka na zawadi ya kombe na fedha taslim Tsh. Milioni kumi (10,000,000), mshindi wa pili Milioni tano (5,000,000), pamoja na zawadi nyengine ambazo zimegawanywa katika makundi tofauti ikiwemo zawadi ya mfungaji bora, mchezaji bora, mwamuzi bora, kipa bora, mwandishi wa habari bora, timu bora na zawadi nyeanginezo.
    Kupitia matandao wako makini wa http://bongostaz.blogspot.com/ tutakuwa ukiwaletea kila kitakachoendelea katika mashindano hayo kuanzia mwanzo mpaka mwisho
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: SIMBA SC YAPANGWA NA TUSKER FC YA KENYA MAPINDUZI CUP Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top