• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 27, 2012

  NIZAR NI MTU WA KUCHEZA YANGA, TENA SANA TU

  Hakuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza cha Yanga katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na mara nyingine amekuwa akimalizia benchi dakika zote za mchezo, kuanzia Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame. Lakini mara zote chache alipoinuliwa kutokea benchi, kiungo Nizar Khalfan amekuwa akionyesha yeye ni mtu anayepaswa kuwa uwanjani muda wote. Hata jana Nizar, alitokea benchi katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Tusker ya Kenya, akacheza soka maridadi, akiwatengenezea wenzake nafasi na hata kujaribu mwenyewe kufunga. Alikuwa anakaba kila timu ilipopoteza mipira na kwa ujumla alikuwa anacheza kwa manufaa ya timu. Huyu ni mchezaji mwenye uzoefu aliyecheza soka ya kulipwa Asia na Amerika. Amecheza Ligi kubwa pamoja na wachezaji kama Thierry Henry na David Beckham nchini Marekani. Amecheza mechi nyingi za kimataifa na amefanya mambo makubwa ya kihistoria, ikiwemo kumtungua bao tamu sana kipa wa Senegal, Tony Silva. Huwezi kuona sababu ya Nizar kuwekwa benchi Yanga.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: NIZAR NI MTU WA KUCHEZA YANGA, TENA SANA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top